Sheikh Jalala alisisitiza umuhimu wa kushikamana na Uislamu sahihi wa Nyumba ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) na kizazi chake kitakasifu, akibainisha kuwa huu ndio msingi wa umoja na mafanikio ya Waislamu.

1 Oktoba 2025 - 12:49

Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania Awaasa Viongozi na Waumini Mkoani Simiyu +Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (TIC), Maulana Sheikh Hemedi Jalala Mwakindenge, akiendelea na ziara yake ya Kanda ya Ziwa pamoja na jopo lake kutoka Dar es Salaam, alipata fursa ya kuzungumza na waumini pamoja na viongozi wa Jumuiya hiyo Mkoani Simiyu.

Katika hotuba yake, Sheikh Jalala aliwahimiza viongozi kuwa na kauli njema na hekima wanapowaongoza Waumini wao, akisisitiza kwamba kiongozi bora ni yule anayejali heshima na utu wa wale anaowaongoza. Vilevile aliwakumbusha kutoacha kuswali katika mwanzo wa wakati, jambo linaloongeza ucha Mungu na mshikamano wa kiroho.

Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania Awaasa Viongozi na Waumini Mkoani Simiyu +Picha

Aidha, Sheikh Jalala alisisitiza umuhimu wa kushikamana na Uislamu sahihi wa Nyumba ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) na kizazi chake kitakasifu, akibainisha kuwa huu ndio msingi wa umoja na mafanikio ya Waislamu.

Kauli mbiu za mkutano huo zilihimiza Umoja, Ushirikiano na Mshikamano wa kiimani kama watu wa Umma Mmoja wa Kiislamu wanaofuata Kitabu kimoja na Mtume Mmoja, Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania Awaasa Viongozi na Waumini Mkoani Simiyu +Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha